NIGERIA-LAGOS

Rais wa Nigeria amfukuza kazi mkuu wa tume ya kupambana na rushwa

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan REUTERS/ Daniel Munoz

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameamua kumtimua Mkuu wa Kitengo Cha Kupambana na Rushwa nchini humo Farida Waziri na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Lamorde kutokana na uwepo wa ukosoaji mkubwa wa kiongozi huyo.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Rais Jonathan umekuja wakati ambapo ripoti ya Shrika la Kutetea Haki za Binadamu ikionesha kuwa Kitengo hicho cha Rushwa kilikuwa kinaongozwa bila kufuata weledi, kuingiliwa kisiasa na kuendelea kwa rushwa iliyokithiri.

Taarifa ya Ikulu ya Nigeria imethibitisha kuanza kwa uteuzi huo mara moja bila ya kubainisha Waziri baada ya kuondolewa kwenye kitengo hicho atapewa kazi gani wakati huu ambapo nchi hiyo ikitajwa kuzingirwa na rushwa.

Toka rais Jonathan aingie madarakani amekuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo vya rushwa huku mara kadhaa akiwabadili kazi mawaziri wake ambao wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Tayari mawaziri kadhaa wa zamani katika serikali yake wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za rushwa ambazo zinawakabili huku wengi wao wakituhumiwa kwa kutumia madaraka vibaya pamoja na kusaini mikataba iliyoitia serikali hasara.