MOROCCO

Wananchi wa Morocco wanapiga kura kuchagua wabunge

Mfalme Mohammed wa Morocco (kulia)
Mfalme Mohammed wa Morocco (kulia) REUTERS/Maghreb Arab Press

Wananchi wa Morocco wanapiga kura ya kuchagua wabunge ukiwa ni uchaguzi wa kwanza kufanyika baada ya kufanyika mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo ambayo yaliongeza nguvu kwa bunge na Waziri Mkuu.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo utashuhudia vyama thelathini na moja vilivyosajiliwa nchini Morocco vikipambana kusaka nafasi za wabunge mia tatu na tisini na tano ambao watakuwa na jukumu la kuwawakilishi wananchi wa taifa hilo.

Hofu imeshaanza kutanda huenda idadi ya wapiga kura ikawa ndogo kutokana na uchaguzi huo kugomewa na wale ambao walifanikisha mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo wakidai kuna masuala bado yamejaa dosari.

Uchaguzi huo unafanyika wakati ambapo baadhi ya wanaharakati walioshiriki katika harakati za kubadilishwa kwa katiba mpya wakigomea kushiriki kwenye uchaguzi huo wakitaka usogezwe mbele kwakile walichodai kuwa mambo mengi yamepuuzwa.

Wanafunzi wa elimu ya juu nchini humo wameitisha maandamano ya nchi nzima wakati wa zoezi la upigaji kura kuwashawishi wananchi kutoshiriki kwenye uachaguzi huo ambao wamesema hawatokubali matokeo yake.