Togo

Ajali ya basi lawaua wachezaji wa soka wa Togo baada ya kuwaka moto

Wachezaji wa mchezo wa soka nchini Togo ni baadhi ya watu sita waliouawa baada ya basi walilokuwa wanasafiria kushika moto kilomita 100 Kaskazini mwa mji mkuu wa Lome siku ya Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Pamoja na wachezaji hao wa klabu ya Etoile Filante waliokuwa wanasafiri kwenda kushiriki katika mchuano wa soka,watu wengine pia waliokuwa ndani ya basi hilo wameripotiwa kujeruhiwa.
 

Ripoti zinaeleza kuwa,kabla ya moto huo kuwaka tairi la basi hilo lilipuka na basi hilo kubingiria kabla la kushika moto.
 

Abiria waliopata majeraha wanapata matibabu katika hospitali ya kijeshi mjini Lome,baada ya rais Faure Gnassingbe kutoa amri ya wao kutibiwa katika hospitali hiyo.

Mwaka uliopita,wachezaji wawili wa timu ya taifa ya soka ya Togo waliuawa baada ya basi walilokuwa wanasafiria kuvamiwa na waasi nchini Angola wakati kombe la mataifa bingwa barani Afrika,a mwaka 2007 waziri wa michezo wa Togo alikuwa miongoni mwa mashabiki 22 wa timu ya taifa ya Togo waliouawa baada ya ndege waliokuwa wanasafiria kuanguka nchini Sierra Leone.