SOMALIA

Al Shabaab yapiga marufuku mashirika ya Misaada nchini Somalia

Eneo la Mpaka kati ya Somalia na Kenya
Eneo la Mpaka kati ya Somalia na Kenya Google Maps

Kundi la wanamgambo wa Al-Shabab nchini Somalia limetangaza kuyapiga marufuku mashirika ya kutoa msaada zaidi ya 16 huku nusu ya mashirika hayo yakiwa ni yale ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ya kundi hilo imesema tangazo hilo litahusu mashirika yote ya misaada yaliyoko katikati na kusini mwa Somalia na kwamba halitaruhusu mashirika hayo kufanya kazi tena kwenye maeneo hayo hatua inayoelezwa itaathiri kwa kiasi kikubwa wananchi katika maeneo hayo.

Miongoni mwa mashirika yaliyotangazwa kupigwa marufuku ni pamoja na shirika linaloshughulikia watoto UNICEF, shirika la Afya WHO, shirika la wakimbizi UNHCR na GTZ.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban ki Moon amelaani hatua ya kundi hilo akiita ni ya kinyama, hatua inayokuja ikiwa ni siku chache zimepita tka majeshi ya kenya na Ethiopia yaingie nchini humo kwa kushirikiana na majeshi ya AMISOM kuwasaka wanamgambo hao.