LIBYA

Taarifa ya Umoja wa Mataifa yasema watu 7000 wanashikiliwa katika Magereza ya nchini Libya

Aliyekuwa kiongozi wa Taifa la Libya, Marehemu Moamar Gaddafi
Aliyekuwa kiongozi wa Taifa la Libya, Marehemu Moamar Gaddafi

Waangalizi wa haki za binaadam kutoka Umoja wa Mataifa UN wametoa ripoti inayoonesha kuwa waasi nchini Libya wanaendelea kuwashikilia zaidi ya wafungwa 7000 ambao wanatuhumiwa kuwa walikuwa wapiganaji wa serikali ya Marehemu Kanali Muamar Gaddafi. 

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa mataifa , serikali ya mpito ya Libya inawashikilia watu hao ambao wengi ni kutoka nchi za kusini mwa Afrika bila hata kuwafungulia mashtaka kitu kinachozusha hofu ya kuwepo ukiukwaji wa haki za binadamau kwa wafungwa hao.

Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali ya libya imeanza kuchukua hatua ya kuanza kuwarejesha katika nchi husika baadhi ya raia ambao wamefahamika uraia wao kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.

Hivi karibuni mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo yalitoa ripoti ya pamoja na kuonesha wasiwasi wao kuhusu hatima ya watu hao kwa kile walichodai kuwa kumekuwepo na taarifa za kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji kwa baadhi ya wafungwa.