MISRI

Uchaguzi nchini Misri waingia siku ya pili hii leo.

Raia wa Misri wakiwa katika zoezi la upigaji kura za Ubunge
Raia wa Misri wakiwa katika zoezi la upigaji kura za Ubunge REUTERS/Ahmed Jadallah

Uchaguzi wa kwanza kufanyika tangu Mapinduzi yalipofanyika nchini Misri, umeingia siku ya pili hii leo huku kukiwa na taarifa za wapiga kura wengi kujitokeza kushiriki zoezi la upigaji kura kuelekea kwenye utawala wa kidemokrasia.

Matangazo ya kibiashara

Kuzaliwa kwa Misri mpya kulitangazwa na gazeti linalomilikiwa na serikali,Al -Akbar hii leo hku magazeti mengine yakiripoti juu ya mbio za raia kuelekea katika demokrasia na upigaji kura ulio huru na la usalama.
 

Raia wa Misri walionekana katika miji ya Cairo na Alexandria wakisubiri katika misururu jana kupiga kura za ubunge, ikiwa ni zoezi la kwanza tangu kuangushwa kwa aliyekuwa mtawala wa Taifa hilo,Hosni Mubarak mwezi Februari.
 

Chama cha kiislam kilichowahi kufungiwa cha Muslim Brotherhood kinatarajiwa kuwa na nguvu kubwa iwapo kitapata ushindi, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi tarehe 13 mwezi wa Januari.
 

Baada ya kutolewa kwa matokeo, nchi hiyo itaingia katika uchaguzi mwingine wa uchaguzi wa Bunge kuu,hata hivyo bado haijajulikana namna Bunge litakavyokuwa likifanya kazi na namna litakavyoweza kujadili na jeshi juu ya mamlaka itakayokuwa nayo baada kuundwa kwa katiba mpya mwakani.