MISRI

Chama cha Muslim Brotherhood huenda kikapata ushindi nchini Misri

Msururu wa Raia wa Misri walipokuwa wakipiga Kura
Msururu wa Raia wa Misri walipokuwa wakipiga Kura REUTERS/Ahmed Jadallah

Chama cha Kiislam nchini Misri kimeelezwa huenda kitapata ushindi na kuliongoza taifa hilo baada ya kura zilizopigwa juzi na jana nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha Muslim Brotherhood, kilichowahi kufungiwa wakati wa utawala wa aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Hosni Mubarak aliyeondolewa madarakani mwezi Februari mwaka huu, kimesema chama cha uhuru na haki ,FJP kinaongoza katika matokeo ya awali.

Mamilioni ya raia wa Misri walitumia uhuru wao wa kidemokrasia na kuwasili katika vituo vya kupiga kura mjini Cairo na Alexandria ili kuchagua Wabunge wao.

Chama cha Muslim Brotherhood limejipatia umaarufu na kutambulika miongoni mwa raia wa Misri kutokana na harakati za kuupinga utawala wa Mubarak na kazi za kusaidia wahitaji.

Vyama vingi vya kisiasa vilivyoibuka baada ya kuondoka kwa Mubarak havifahamiki na wapiga kura huku vingine vikikosa umoja miongoni mwao.
 

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, Abdel Moaz Ibrahim amesema matokeo ya awamu ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge kutoka majimbo tisa yatatangazwa kesho jioni.