HAGUE

Gbagbo awasili Uholanzi kupandishwa katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC

Aliyekuwa Rais wa Cote d Ivoire, laurent Gbagbo alipotiwa nguvuni nchini humo
Aliyekuwa Rais wa Cote d Ivoire, laurent Gbagbo alipotiwa nguvuni nchini humo AFP/TCI

Aliyekuwa rais wa Cote d' Ivoire Laurent Gbagbo amepelekwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kukabiliana na shutma za ukiukaji wa haki za Binaadam uliotokea nchini humo baada ya uchaguzi wa rais.

Matangazo ya kibiashara

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC Luis Moreno Ocampo, amesema kuwa Gbagbo ni mtu wa kwanza kushtakiwa kuhusika na machafuko ya nchini Cote d' Ivoire yaliyasababisha watu zaidi ya elfu tatu kupoteza maisha.

Gbagbo aliwasili mjini Hague akitokea Cote d' Ivoire alikokuwa akishikiliwa tangu mwezi Aprili mwaka huu.

Gbagbo anahusishwa na makosa ya mauaji, ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia, vitendo vilivyotekelezwa kati ya tarehe 16 mwezi Desemba mwaka jana na tarehe 12 mwezi Aprili mwaka huu baada ya kukataa kuachia madaraka mara baada ya Allasane Ouattara kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa urais nchini humo.

Ocampo amewaahidi waathiriwa wa matukio ya machafuko nchini humo kuwa wataona haki inatendeka na kuahidi kuwa watuhumiwa wengine zaidi watapelekwa mbele ya mkono wa sheria.