CONGO

Upinzani walalamikia uchaguzi wa CONGO kujawa na udanganyifu

Zoezi la kuhesabu kura likiendelea DRC
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea DRC Daniel Finnan

Waangalizi wa uchaguzi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wagombea wa nafasi ya urais wamedai kuwa uchaguzi huo ni batili. 

Matangazo ya kibiashara

Wakielezea hali hiyo waangalizi wa ndani na wa kimataifa wamesema kuwa kumekuwa na ucheleweshwaji wa masanduku na karatasi za kupigia kura huku mamilioni ya wapiga kura wakiondoka kwenye vituo vya kupiga kura

kumekuwa na madai ya kubatilishwa kwa kura hizo, wakidai kuwa zilijawa na udanganyifu,huku Rais wa tume ya uchaguzi Daniel Ngoy Mulunda akipinga madai hayo ya upinzani juu ya shutma dhidi ya tume hiyo.

Tume ya uchaguzi imekuwa ikikosolewa wakati wote tangu maandalizi ya kura hizo kwa kufanya kazi nyuma ya Ratiba ilipokuwa ikijaribu kupambana na changamoto za maandalizi.

Matokeo ya awali ya uchaguzi yanatarajiwa kutolewa tarehe 6 mwezi ujao.