Senegal

Mwanamuziki Youssou Ndour atangaza kuwania urais nchini Senegal

DR

Ikiwa ni miezi miwili tu imesalia kwa nchi ya Senegal kufanya uchaguzi wake mkuu, watu mbalimbali wameanza kutangaza nia ya kuwania kiti cha urais kupambana na rais Abdoulaye wade, ambapo safari hii mwanamuziki mkongwe nchini humo Youssou Ndour ametangaza kuwania urais.

Matangazo ya kibiashara

Akitumia kituo chake cha Televisheni, mwanamuziki Ndour ambaye hivi karibuni aliunda chama chake mwenyewe, amesema kuwa atasimama kuwania urais wa nchi hiyo huku akitajwa kuwa moja kati ya wagombea ambao wanatarajiwa kutoa upinzani mkali kwa rais Wade.

Licha ya kukosolewa na wapinzani wake, wasomi pamoja na wanasiasa kuwa hakupata elimu ya juu, Ndour amesisitiza kuwa hicho sio kigezo cha kumfanya yeye asigombee urais kwakuwa nafasi ya urais sio kazi bali ni uongozi.

Ndour amesema kuwa kampeni zake zitajumuisha juhudi za kuleta amani katika eneo la mji wa Casamance, utawala bora na miradi ya maendeleo ya jamii na kilimo