Sudani Kusini

Maelfu ya Raia wa Sudani Kusini wahitaji msaada wa haraka:UN

Rais wa Sudan Omary Bashir akiwa na rais wa Sudani Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Omary Bashir akiwa na rais wa Sudani Kusini Salva Kiir UN Photo/Isaac Billy

Umoja wa mataifa umesema kuwa Maelfu ya raia wa Sudani Kusini waliokimbia machafuko katika jimbo la Jonglei wanahitaji msaada wa haraka.

Matangazo ya kibiashara

Mratibu wa shughuli za maswala ya misaada ya kibinaadam kutoka umoja wa mataifa huko sudani kusini Lise Grande amesema msaada utahitajika wiki zijazo kwa ajili ya watu walioathirika na machafuko.
 

Takriban vijana 6,000 wa kabila la Lou Nuer wenye silaha wiki iliyopita walivamia mji wa Pibor, makazi ya mahasimu wao,watu wa kabila la Murle wanaodai kuwa wezi wa ng'ombe wao .
 

Watu wenye silaha wamechoma moto makazi na kuvamia hospitali na zahanati zinazoendeshwa na madaktari wasio na mipaka huku taarifa zikisema kuwa zaidi ya watu 1,000 wameuawa katika miezi ya karibuni huku hali hiyo ikiteteresha usalama wa taifa hilo.