LIBYA

Wananchi Libya waadhimisha kumbukumbu ya maandamano yaliyomng'oa Gaddafi

REUTERS/Ismail Zitouny

Raia nchini Libya hii leo wanasherekea kumbukumbu ya maandamano yaliyoangusha utawala wa aliyekuwa Kiongozi wa Taifa hilo, Marehemu Muammar Gaddafi mwaka mmoja uliopita.

Matangazo ya kibiashara

waasi wa zamani waliokuwa wakisaidiwa na Majeshi ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO wameweka vituo vya ukaguzi mjini Tripoli, Benghazi, Misrata na miji mingine.

Viongozi wapya nchini humo hawajaandaa sherehe zozote kitaifa kwa ajili ya kutoa heshima na kuwakumbuka maelfu ya watu waliouwa katika machafuko nchini humo yaliyosababisha kukamatwa kwa Gaddafi tarehe 20 mwezi Octoba mwaka jana.

Kumbukumbu hizo zinatarajiwa kufanywa na wakazi wa miji mbalimbali nchini humo wakiongozwa na wakazi wa mjini Benghazi, mji ambao ni wa kwanza kuanzisha mapinduzi dhidi ya utawala uliodumu kwa miaka 42.

Wakazi hao wameandaa sherehe hizo za kumbukumbu ambazo zinatarajiwa kuhudhuriwa na na kiongozi mpya wa Taifa hilo, Mustafa Abdel Jalil na waziri Mkuu wa Serikali ya mpito Abdel Rhim al -KIB na vionlgozi wengine.
Abdel Jalil ameonya kuwa moyoa wa kimapinduzi wa Libya na uthabiti wake hautaingiliwa kwa namna yeyote ile na kuwa serikali yake imewapokea watu wote waliounga mkono Mapinduzi na ambao hawakuyaunga mkono