Sudani-Darfour

Hatimaye waasi wa kundi la JEM wawaacha huru wafanyakazi 40 waliokuwa wakiwashikilia

Waasi wa Darfour
Waasi wa Darfour

Waasi wa Justice and Equality Movement JEM wenye maskani yao katika Jimbo lenye machafuko la Darfur nchini Sudan hatimaye wametangaza kuwaachia wafanyakazi arobaini na tisa wanaofanyakazi ya kulinda amani katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Kundi la Waasi la JEM Gibril Adam Bilal amethibitisha kuachiwa kwa wafanyakazi hao arobaini na tisa ambao walikamatwa mapema siku ya jumatatu lakini bado wanaendelea kuwashikilia wanajeshi wa tatu wa Sudan.

Gibril amesema wanaendelea kuwashikilia wanajeshi hao watatu huku wakifanya uchunguzi kama wanahusika na masuala ya kiusalama