Tunisia

Chama madarakani nchini Tunisia chapinga mfumo wowote wa sharia

Maandamano ya wafuasi wa Salafiste wakidai mfumo wa sheria nchini Tunisia
Maandamano ya wafuasi wa Salafiste wakidai mfumo wa sheria nchini Tunisia REUTERS/Zoubeir Souissi

Chama cha kiislamu chenye mrengo wa kati nchini Misri cha Ennahda ambacho kinaongoza serikali ya Tunisia kimetangaza wazi kuwa kitapinga kifungu chochote kwenye katiba mpya ya nchi hiyo ambacho kitataka kutambua utawala wa Sharia.

Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa viongozi wa chama hicho Ameur Larayed, amesema kuwa chama chake kinapinga kwa nguvu zote chama chochote ambacho kitataka kuingizwa kwa sharia kwenye katiba ya nchi hiyo na kuwa kama sheria mama za nchi.

Katika taarifa ya chama hicho imesema kuwa kuingiza sharia kwenye katiba mpya ni kutaka kubadili taifa hilo kuwa la kiislamu jambo ambalo kimesema kwa dunia ya sasa sio rahisi.

Kiongozi wa chama hicho Rachid al-Ghannouchi, amesema kuwa chama chake kitaendelea kutambua katiba ya nchi hiyo ambayo inatambua taifa la Tunisia kama taifa la kiislamu lakini halitatambua mfumo wa shari.