MALI

Makaburi yaliyoko kwenye orodha ya urithi wa Dunia kaskazini mwa nchi ya Mali yachomwa moto

Askari wa wafuasi waliouteka mji wa Timbuktu wakiwa kwenye doria kaskazini mwa nchi hiyo
Askari wa wafuasi waliouteka mji wa Timbuktu wakiwa kwenye doria kaskazini mwa nchi hiyo Reuters

Wafuasi wa kundi la Al-Qaeda nchini Mali wamvamia mji wa Timbuktu ulioko kaskazini mwa nchi hiyo na kucoma moto makaburi ya kumbukumbu ya viongozi wa dini ya kiislamu kwenye mji eneo ambalo pia limetajwa kuwa ni kumbukumbu za dunia.

Matangazo ya kibiashara

Uvamizi wa eneo hilo umeendelea kuzusha hofu ya mapigano kati ya wenyeji wa mji wa Timbuktu na waislamu waliouteka mji huo mwezi April kwakile kilichoelezwa kuwa wakazi wa mji huo wamekuwa wakitumia makaburi hayo kwa ibada.

Kaburi hilo la kiongozi wa kidini, Sidi Mahmoud Ben Amar limeelezwa kuchomwa moto na wafuasi wa Ansar Dine ambao walifika kwenye eno hilo kwaajili ya maombi lakini baadae waliamua kuchoma moto.

Msemaji wa kundi hilo, Sanda Ould Boumama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukanusha kuhusika na uchomaji moto wa kivutio hicho cha dunia.

Kaburi la Sidi Mahmoud Ben Amar ni miongoni mwa makaburi 16 yaliyoorodheshwa kidunia na shirika la umoja wa mataifa la UNESCO kuwa sehemu ya urithi wa dunia ambao unamakaburi zaidi ya 333 kwa wakati mmoja.

Viongozi wa kidini nchini Mali wameitaka serikali kulaani kitendo kilichofanywa na wafuasi hao na kutaka kuchukua hatua dhidi ya waliohusika.

Hata hivyo mashuhuda watukio hilo wamesema kuwa sio mali zote zilizokuwa kwenye makaburi hayo ziliteketea kwa moto.