NIGERIA

Serikali ya Nigeria yawafukuza kazi madaktari waliokuwa kwenye mgomo

Madaktari nchini Nigeria wakiwa kwenye mgomo
Madaktari nchini Nigeria wakiwa kwenye mgomo Reuters

Mamlaka jijini Lagos nchini Nigeria imewafuta kazi wafanyakazi madaktari waliokuwa katika mgomo wakidai malipo ya mishahara kwa kipindi cha majuma matatu yaliyopita. 

Matangazo ya kibiashara

Jumla ya madaktari 788 waliokuwa wakifanya kazi serikalini wafutwa kazi wakidaiwa kufanya mgomo usio halali ulioanza tangu Aprili 16 mwaka huu.

Kufukuzwa kazi huko kumesababishwa na kile kilichoelezwa madaktari kukaidi kujibu swali la kwa nini hawakuwepo kazini bila kupewa taarifa na ruhusa ya likizo na bila kufuata sheria zihusuzo migomo kazini.

Serikali ya Nigeria imeajiri madaktari 373 kufidia waliofukuzwa kazi na zoezi la kuajiri wengine litaendelea hivi karibuni.

Madaktari hao waliingia kwenye mgomo usio na kikomo wakidai nyongeza ya mshahara pamoja na marupurupu ambayo serikali ya nchi hiyo ilikuwa imeahidi kuwapatia katika kipindi cha nyuma.

Nchi nyingi barani Afrika zimejikuta zikikumbwa na migomo ya madaktari ambao wameendelea kuzishinikiza serikali zao kuwapatia maslahi bora wawapo kazini.