GUINEA

Upinzani nchini Guinea kuitisha maandamano ya nchi nzima kushinikiza Serikali kuitisha uchaguzi mkuu

Le président guinéen Alpha Condé
Le président guinéen Alpha Condé Reuters

Viongozi wa upinzani nchini Guinea wametangaza kufanya maandamano ya kitaifa tarehe 10 mwezi huu, kushinikiza kufanya mazungumzo na serikali ya Rais wa nchi hiyo, Alfa Conde kuhusu ucheleweshwaji wa kufanyika uchaguzi wa Ubunge. 

Matangazo ya kibiashara

Akiongea na vyombo vya habari ,Kiongozi wa chama cha upinzani cha UNION OF DEMOCRATIC FORCES OF GUINEA Cellou Dalein Diallo amesema wameamua kufanya maandamano kuwasilisha madai yao na wataendelea hivyo mpaka watakaposikilizwa.

Uchaguzi wa awali uliahirishwa mwezi Aprili, kwa kile Conde alichodai mapungufu ya kiufundi ambayo yalikuwa nje ya uwezo wao.

Kwa Mujibu wa Katiba ya Guinea,Uchaguzi wa wabunge ulitakiwa kufanyika ndani ya miezi sita ya kusimikwa Rasmi kwa Conde mwezi Desemba mwaka 2010.

Uchaguzi wa Ubunge wa mwisho kufanyika ulikuwa mwezi June mwaka 2002 kipindi cha utawala wa Lansana Conte aliyefariki mwezi December mwaka 2008 baada ya kuwa madarakani kwa miaka 24.