NIGERIA

Mtu mmoja anaedhaniwa kuwa mfuasi wa kundi la Boko Haram auawa nchini Nigeria

Moja ya shambilio ambalo limefanywa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria
Moja ya shambilio ambalo limefanywa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria REUTERS/Stringer

Mtu mmoja anayedaiwa kuwa mfuasi wa kundi lenye msiamamo mkali la Boko Haram ameuawa na wengine wamejeruhiwa na Wanajeshi Mjini kaskazini mashariki mwa Nigeria baada ya kushambuliana kwa Risasi. 

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Jeshi nchini humo amesema hakuna mwanajeshi wala Raia aliyeuawa au kujeruhiwa katika shambulio hilo.

Mji wa Maiduguri ulio kwenye jimbo la Borno ni makazi ya Boko Haram , ambapo kumeshuhudiwa machafuko ambayo yameelezwa kutekelezwa na kundi hilo ambalo limekuwa likielekeza mashambulizi yake Kaskazini mwa Nigeria.

Kundi la Boko Haram limeendelea kujiapiza kufanya mashambulizi zaidi nchini humo ambapo hivi karibuni wapiganaji wake wamekuwa wakilenga ofisi za vyombo vya habari.

Juma lililopita msemaji wa kundi hilo alitangaza vita dhidi ya baadhi ya vyombo vya habari nchini humo ambavyo vimekuwa upande wa Serikali na kudai kuwa wanajiandaa na mashambulizi zaidi.

Boko Haram wanashutumiwa kusababisha zaidi ya watu 1000 kupoteza maisha tangu katikati ya mwaka 2009.