Algeria

Chama cha kiislam Nchini Algeria chatishia kufanya Mapinduzi kama ya Tunisia

Chama Cha Kiislam nchini Algeria kimetishia kuchukua hatua za kimapinduzi kama ambazo zilifanyika nchini Tunisia wakiamini hiyo ndiyo njia pekee ya kupata haki yao baada ya kuona kisanduku cha kura kimeshindwa kufanya kazi.

Rais wa Algeria Abdul Aziz Bouteflika
Rais wa Algeria Abdul Aziz Bouteflika Reuters/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Chama Cha Kiislam nchini Algeria Abdllah Djaballah ametoa kitisho hicho baada ya kushuhudia chama cha Rais wa nchi hiyo kikipata wingi wa wabunge kwenye uchaguzi uliofanyika juma lililopita.
 

Djaballah amesema matokeo haya yamefunga mlango wa mabadiliko ambao wakuwa wanautegemea kupitia uchaguzi na hatimaye wangepata utawala mpya ambao umekuwa ukisubiriwa kwa hamu na wananchi.
 

Chama cha Rais Abdelazizi Bouteflika cha NLF kimeganikiwa kupata wingi wa viti katika ya vile mia mbili na ishirini vilivyokuwa vinawaniwa huku chama cha Kiislam kikiambulia viti hamsini na kenda pekee.
 

Kiongozi wa Chama Cha Kiislam amesema kuna kila dalili ya mchezo wa wizi wa kura ambao umefanyika ili kuhakikisha chama cha Rais Bouteflika kinashinda uchaguzi na kuendelea kutawala nchini hiyo kwa muda zaidi.