Sudani Kusini

Raia takriban elfu kumi na mbili wa Sudani kusini wawasili Mjini Juba kutokea Sudani

Rais wa Sudan Omary Bashir akiwa na rais wa Sudani Kusini Salva Kiiri
Rais wa Sudan Omary Bashir akiwa na rais wa Sudani Kusini Salva Kiiri UN Photo/Isaac Billy

Kundi la kwanza la raia zaidi ya elfu kumi na mbili wa Sudan kusini limewasili mjini Juba jana jioni wakitokea Khartoum ambako serikali ya nchi hiyo ilitangaza kuwafukuza.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Kahrtoum iliwataka raia wote wa Sudan kusini kuondoka nchini humo na kurejea nchini mwao, hatua iliyokuja siku chache baada ya Sudan Kusini kujitenga toka serikali ya Khartoum na kuwa taifa huru.

Mpango wa kuwarejesha nyumbani raia hao unasimamiwa na shirika la umoja wa mataifa linalosimamia wahamiaji IOM ambapo limeandaa ndege maalumu zinazowachukua wananchi wa Sudan Kusini walioko Khartoum na kuwarejesha nyumbani.

Maelfu ya wananchi wa Sudan kusini waliokuwa wanaishi Khartoum walipoteza ajira zao pamoja na haki za makazi na kuachwa bila vibali maalumu vya ukaazi hali ilichochea chuki baina ya mataifa hayo mawili.