Congo

Serikali ya Congo yasisitiza nia yake ya kumfikisha Jenerali Jean Bosco Ntaganda kwenye Mahakama ya ICC

Kiongozi wa Jeshi la waasi anayesakwa na ICC, Jenerali Bosco Ntaganda
Kiongozi wa Jeshi la waasi anayesakwa na ICC, Jenerali Bosco Ntaganda © CPI

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC imesema bado mpango wake wa kumkabidhi Kiongozi wa Waasi Jean Bosco Ntaganda kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC kutokana na kutendo makosa ya kivita upo pale pale. 

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Serikali ya DRC Lambert Mende ametoa kauli hiyo saa kadhaa baada ya Kiongozi wa Mashtaka wa Mahakama ya ICC Luis Moreno-Ocampo kutamka anataka kuangalia makosa mengine ambayo yamefanywa na Bosco Ntaganda na Sylvestre Mudacumura.

Moreno-Ocmapo amesema huu ni wakati muafaka kwa wanajeshi wa Rwanda na Congo kwa pamoja kuendesha operesheni ya kuwakamata Waasi hao ambao wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji na ubakaji.

Katika hatua nyingine,Familia zilizokimbia makazi yao zimeanza kurejea Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuwepo kwa hali ya utulivu, katika maeneo ya Rutshuru, katika Mpaka wa Rwanda na Uganda.

Jeshi la nchi hiyo liliingia katika mapigano na waasi juma lililopita baada ya muda wa makataa kuisha wa kuwataka waasi hao kurudi katika jeshi la Serikali.