Kenya

Mtu mmoja auawa kwa Shambulio la Guruneti katika Mgahawa mmoja Jijini Mombasa

Moja ya Mashambulizi ya Guruneti iliyokumba Jiji la Nairobi
Moja ya Mashambulizi ya Guruneti iliyokumba Jiji la Nairobi EUTERS/Noor Khamis

Mtu mmoja ameuawa baada ya shambulio la Guruneti kutokea Mjini Mombasa, Polisi wamethibitisha hii leo ikiwa siku moja baada ya watu wenye silaha kushambulia na kurusha milipuko katika mgahawa mmoja.

Matangazo ya kibiashara

Aliyeuawa katika Shambulio hilo ni Mwanamke ambaye alikuwa Mlinzi katika kilabu, huku watu watatu waliojeruhiwa katika shambulio hilo wanaelezwa kuwa bado wako hospitalini, mmoja kati yao akiwa mahututi.
 

Mtu mmoja alifyatua risasi baada ya Walinzi katika mgahawa uitwao Bella Vista kumzuia mtu huyo na wenzake wawili kuingia katika Mgahawa kabla ya watu hao kurusha maguruneti mawili na kukimbia.
 

Mgahawa huo ni Maarufu sana katika Mitaa Mbalimbali ya Mjini Mombasa na mara kwa Mara Watalii wamekuwa wakitembelea Mgahawa huo.
 

Hakuna taarifa zilizotolewa juu ya wahusika wa shambulio hilo.
 

Tangu Kenya ilipopeleka Vifaru vyake na Majeshi yake Nchini Somalia Mwaka jana , Nchi hiyo imekumbwa na Mfullizo wa mashambulizi Jijini Nairobi , katika Miji ya Kaskazini mwa Nchi hiyo halikadhalika katika Kambi za Wakimbizi wa Kisomali karibu na Mpakani.