Sudani

Mpatanishi wa Mgogoro wa Sudan na Sudani kusini Thabo Mbeki kuwasili Khartoum hii leo

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir akizungumza na waandishi wa habari
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir akizungumza na waandishi wa habari UN Photo/Isaac Billy

Mpatanishi wa Mgogoro wa Sudan na Sudani Kusini kutoka Umoja wa Mataifa, Thabo Mbeki hii leo anatarajiwa kuwasili Mjini Khartoum kusaidia kuzishawishi nchi hizo kurudi tena kwenye Mazungumzo ambayo yaliahirishwa baaada ya Mapigano katika Mpaka wa nchi hizo Mwezi uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo zilishindwa kutekeleza matakwa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kuanza tena kwa Mazungumzo, lakini Mbeki na wanadiplomasia wengine wanafanya jitihada za kuhakikisha mazungumzo yanarejea.
 

Rais huyo wa zamani wa Afrika kusini atakutana na Rais wa Sudan, Omar al Bashir na Maafisa wengine na baadae anatarajiwa kutembelea juba, Sudani kusini.
 

Mnamo May 2, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliipa Sudan na Sudani kusini majuma mawili ya kurejea kwenye mazungumzo kwa sharti la kuwekewa vikwazo iwapo watapuuza Pendekezo hilo.
 

Azimio la Umoja wa mataifa lilitaka pande mbili kuacha mapigano na kurejea katika meza ya mazungumzo kijadili maswala yaliyoleta tofauti ya mataifa hayo baada ya kujitenga kwa Sudani Kusini mwezi July Mwaka jana.
 

Msemaji wa Serikali ya Sudani Kusini, Barnaba Marial Benjamin ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa, AFP hii leo kuwa Sudan iko tayari kwa mazungumzo isipokuwa Mbeki hajawaalika kwa ajili ya Mazungumzo kwa kuwa Khartoum imekuwa ikisita.