Mali

Viongozi toka ECOWAS kuijadili Mali na Guinea-Bissau siku ya Jumamosi

Kiongozi wa Jeshi lililopindua Serikali ya Mali, Kapteni Amadou Sanogo.
Kiongozi wa Jeshi lililopindua Serikali ya Mali, Kapteni Amadou Sanogo. REUTERS/Joe Penney

Mawaziri kutoka jumuia ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi watakutana siku ya Jumamosi kujadili jitihada za kurejesha utawala wa kidemokrasia Nchini Mali na Guinea Bissau baada ya tawala za nchi hizo kupinduliwa.

Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa Mambo ya nje na wa ulinzi kutoka mataifa 15 wanachama wa ECOWAS watahudhuria Mkutano wa dharura jijini Abidjan nchini Cote d Ivoire

Mkutano huo utajadili hali ya Usalama na siasa za Mali na Guinea Bissau ambao unakuja baada ya kufanyika Mkutano wa Mawaziri Ulinzi jijini Abuja nchini Nigeria.
 

Viongozi hao waliamua katika Mkutano wa Aprili 26 kupeleka kati ya vikosi 500 na 600 kutoka katika nchi takriban nne, Nigeria, Togo, Cote d Ivoire na Senegal kuelekea nchini Guinea-Bissau
 

Nigeria ilisema kuwa inasubiri maelekezo zaidi kutoka ECOWAS kabla ya kupeleka vikosi nchini Mali, ambapo Jumuia hiyo imekuwa ikijaribu kuondoa Mgogoro wa kisiasa juu ya mtu atakayeongoza Serikali ya Mpito nchini humo.