Congo

Waasi wa Rwanda waua Watu 50 Mashariki mwa Congo:UN

Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila
Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila

Kundi la Wapiganaji la Waasi kutoka nchini Rwanda la FDLR lenye maskani yake kwenye misitu iliyopo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC limefanya mauaji ya watu hamsini Mashariki mwa DRC katika kipindi hiki cha mwezi May pekee Umoja wa Mataifa UN umethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Watu ishirini na wawili kati ya hao hamsini ni wale ambao wameuawa katika Kijiji Cha Kamananga kilichopo Kivu Kusini wakati huu ambapo mashambulizi yao yakisababisha vifo vya watu wengine saba wakiwemo raia na wanajeshi wa Jeshi la DRC.

Matukio haya yanatotekelezwa na FDLR yamesababisha wananchi wengi wa DRC kuyakimbia makazi yao na kuomba hifadhi nchini Uganda.

Niabu Mwenyekiti wa Shirika la Kiraia huko Kivu Kaskazini Omari Kavota amethibitisha kutokea kwa mashambulizi ya FDLR

Mwenyekiti wa Shirika la Kiraia nchini humo, Omari Kavota akizungumza na RFI Kiswahili amekiri kutokea kwa Matukio hayo na kuongeza kuwa hali ya Usalama ni tete katika baadhi ya maeneo.