Mali

Vikosi vya Mali vyashutumiwa kuwekea vikwazo juhudi za kurejesha utawala wa kikatiba nchini humo

Kiongozi wa Jeshi lililopindua Serikali ya Mali, Kapteni Amadou Sanogo
Kiongozi wa Jeshi lililopindua Serikali ya Mali, Kapteni Amadou Sanogo Images de la télévision malienne.

Jumuia ya kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika, ECOWAS,hii leo imewashutumu Wanajeshi walioongoza mapinduzi nchini Mali kwa kuwekea Vizingiti jitihada za kurejesha utawala wa Kikatiba nchini humo. 

Matangazo ya kibiashara

Kushindikana kwa mazungumzo na waasi hao ambao awali walikubali kurudisha utawala wa kiraia kumefanya matumaini ya kufikia Mwafaka kuwa hafifu.

Waziri wa mambo ya nje wa Cote d' Ivoire, Daniel Kablan Duncan ameuambia mkutano wa mawaziri wa ECOWAS kuwa vikwazo hivyo vimewekwa na Majeshi hayo na kufanya mchakato wa kisiasa ulioanzishwa na Jumuia hiyo kuchelewa kutekelezwa.

Mawaziri wa Jumuia hiyo watakutana tena kesho kuijadili Mali halikadhalika juu ya mgogoro wa Guinea Bissau,ambapo Serikali yake ilipinduliwa Mwezi Aprili.