Marekani-NATO

Viongozi wa Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi NATO kujadili kuhusu hatma ya Afghanistani

Ma Rais wa Ufaransa Frncois Hollande na Barack Obama wa Marekani
Ma Rais wa Ufaransa Frncois Hollande na Barack Obama wa Marekani

Viongozo wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO wamekutana kando ya mkutano wa nchi tajiri duniani G8 unaendelea huko nchini Marekani, na kuzungumzia mustakabali wa nchi ya Afghanistani, swala ambalo linaonekana kuzua tofauti kati ya viongozi hao hasa kuhusu uwezo wa jeshi la Afghanistani wa kudhibiti usalama wa raia baada ya kuondoka kwa vikosi vya NATO nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Kabla hata ya mkutano huo kuzinduliwa, Rais wa Ufaransa Francois Hollande amefahamisha kuwa vikosi vyake vitaondoka nchini humo mwishoni mwa mwaka huu tuliomo, miaka miwili kabla ya muda uliopangwa Marekani, na kuongeza kuwa swala hili halingoji tena mjadala.

Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema kuwa anamatumaini kuwa nchi za Jumuiya ya kujihami NATO wataendelea kudhihirisha mshikamano wao licha ya hatuwa ya Ufaransa kuondowa vikosi vyake mapema.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekumbusha viongozi wenzake kamba, walipochukuwa uamuzi wa kuelekea nchini Afghanistani walishirikiana na kwenda pamoja, hivo wanatakiwa pia kushirikiana katika kuondoka nchini humo.

Rais wa Marekani Barack Obama baada ya kukutana ana kwa ana na rais wa Afghanistani Hamid Karzai, amesema kwamba vita vimekwisha nchini Afghanistani, lakini wataendelea  kuiunga mkono nchini hiyo kwa hali na mali.

Upande wake rais wa Afghanistani Hamid Karzai ameipongeza serikali ya Marekani kuhusu mchango wake katika kuhakikisha usalama unaimarika, na kwamba Afghanistani inaharaka ya kutaka kubadili sura ya kuonekana kuwa mzigo kwa jamii ya kimataifa.