MALI-ECOWAS

Viongozi wa Mali waafikiana na ECOWAS kuhusu kipindi cha mpito

Kiongozi wa mapinduzi nchini Mali Hamadou Haya Sanogo, na wajumbe wa ECOWAS
Kiongozi wa mapinduzi nchini Mali Hamadou Haya Sanogo, na wajumbe wa ECOWAS

Hatimae viongozi nchini Mali waafikiana kuhusu kipindi cha mpito. Viongozi wa mapinduzi nchini humo pamoja na wapatanishi kutoka Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS wamefikia muafaka jijini Bamako mji mkuu wa Mali. Kipindi cha mpito kinachoongozwa na rasi Dioncounda Traore kitadumu muda wa miezi kumi na mbili, utaoamalizika na uchafuzi mkuu wa rais. Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi machi 22 Kapteni Amadou Haya Sanogo amepewa hadhi ya rais wa zamani wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Wapatanshi wa ECOWAS wamesema kuridhishwa na hatuwa hiyo ya kipindi cha mpito nchini Mali kitachoanza Mei 22 na kuongozwa na Dioncounda Traore.
Mbali na hatuwa hiyo iliofikiwa, kiongozi wa mapinduzi Kapteni Amadou Sanogo, amepewa hadhi ya kuwa rais wa zamani wa Mali, huku wenzake wakipewa msamaha wa kutofuatiliwa na vyombo vya sheria.

Mkataba huo, uliosainiwa baina ya wasuluhishi, rais wa Mali Dioncounda Traore na waziri wake mkuu Cheikh Modibo Keita umepanga kujuwa hatma ya wanajeshi wengine wa mapinduzi katika kipindi cha mpito ambapo wanajeshi hao wanakibarua kigumu cha kuyakomboa maeneo ya kaskazini yaliomikononi mwa waasi wa MNLA.

Kinacho subiria kwa sasa ni kuona mchango wa kila mmoja katika kipindi cha mpito katika kuepusha mkanganyiko. Rais Dioncounda Traore, waziri mkuu.