LIBYA

Mlipuaji wa ndege ya Lokerbie azikwa nchini Libya

CNN.com

Abdel ali Mohmet al Megrahi, mtu pekee aliyehukumiwa kifungo baada ya kuhusika katika tukio la shambulio la bomu mwaka 1988 katika anga la mjini Lockerbie nchini Scotland amezikwa karibu na mji wa Tripoli nchini Libya.

Matangazo ya kibiashara

Mazishi hayo yalifanyika kimya kimya tofauti na shamrashamra alizozipokea kutoka kwa aliyekuwa Kiongozi wa Libya Marehemu Kanali Moamar Gadafi ambaye alimkaribisha Megrahi aliporejea kutoka kifungoni Scotland baada ya kutumikia kifungo cha miaka nane kabla ya kuachwa huru.

Mazishi hayo yameelezwa kutohudhuriwa na maafisa wa Serikali na wala hakukuwa na wawakilishi kutoka katika Baraza la Mpito la nchi hiyo.

Megrahi amefariki miaka 11 baada ya kuhukumiwa kwa makosa ya kuhusika na tukio la kulipua ndege katika anga la Uskoti mjini Lockerbie mwezi tarehe 21 Disemba, mwaka 1988 na kusababisha watu 259 kupoteza maisha.