Mwanamke wa kwanza aula FIFA ni raia wa Burundi

REUTERS/Arnd Wiegmann

Shirikisho la soka duniani, FIFA limemteua Lydia Nsekera kuwa mwanamke wa kwanza kwa kamati yake kuu ili kuimarisha safu ya uongozi katika shirikisho hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mpaka anateuliwa kushika nafasi hiyo, Lydia Nsekera ni rais wa shirikisho la soka la Burundi.

Mwanamama huyo ambaye amepewa heshima kubwa kimichezo atashikilia wadhifa huo mpya kwa mwaka mmoja hadi utakapofanyika uchaguzi rasmi mwaka 2013.

Katika hatua nyingine shirikisho hilo limemteua raia mmoja kutoka Uswisi Domenico Scala kuongoza kamati mpya ya uhasibu inayolenga kusimamia matumizi ya FIFA.