MALI

Serikali ya mpito Mali sasa katika wasiwasi wa kufikia malengo

REUTERS/Adama Diarra

Mchakato wa mwaka mmoja wa kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kidemokrasia nchini Mali umeanza kwa dosari jana kufuatia kuwapo kwa hali ya wasiwasi kuwa Mchakato huo huenda usifikie malengo yake.

Matangazo ya kibiashara

Wasiwasi huo unakuja baada ya Rais wa Mpito nchini humo Dioncunda Traore kushambuliwa na waandamanaji.

Wapatanishi toka Jumuia ya kiuchumi ya nchi za Magharibi, ECOWAS wametishia kuwawekea vikwazo wale waliohusika na shambulio dhidi ya Rais huyo hali inayooelezwa kuwa imeteteresha mpango wa makubaliano yaliyofikiwa.

Mkuu wa tume ya ECOWAS, Kdre Desire Ouedraogo amesema tume itafanya uchunguzi kuwabaini waliomshambulia Traore na kuwawekea vikwazo na kuwachukulia hatua.

Shambulio lililotekelezwa limekemewa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Bunge la Mali, wote wakitaka Mamlaka kuhakikishia usalama maafisa wa Serikali ya Mpito.

Shambulio hilo dhidi ya rais wa mpito nchini Mali limelaaniwa na jumuiya kimaitaifa, ECOWAS na kapteni Sanogo ambaye aliongoza mapinduzi dhidi ya serikali kabla ya kuingia katika uongozi wa mpito unaolenga kuirejesha nchi katika utawala wa kikatiba na demokrasia.