Sudan Kusini

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir asema dola Bilioni 4 zimeibiwa na maafisa wa serikali yake

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema Dola Bilioni 4 zimeibiwa katika serikali yake, katika kashfa ya ufisadi ambayo imenza kutikisa taifa hilo changa.

Matangazo ya kibiashara

Rais Kiir ametaka fedha hizo kurudishwa huku akionesha masikitiko makubwa kwa fedha hizo kupotea bila kufahamika vema ni vipi zilivyotumika.

Hata hivyo,rais Kiir hajaeleza ikiwa fedha hizo ziliibiwa au la lakini amewaandikia barua maafisa wakuu katika serikali yake kuwataka kurejesha fedha hizo.

Benki ya dunia ilionya wiki iliyopita kuwa, Juba inaelekea pabaya kiuchumi ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa kuokoa uchumi wake.

Uchumi wa Juba umekuwa ukikumbwa na hali ngumu kutokana na machafuko katika mpaka wake na Sudan kutokana na mzozo wa mmiliki wa visima vya mafuta.

Mazungumzo kati ya Khartoum na Juba yanaendelea mjini Addis Ababa Ethiopia, kujaribu kutafuta suluhu la kudumu baina ya matufa hayo mawili.

Kwingineko,raia wa Sudan Kusini wanatarajiwa kuanza kurejea nyumbani kufikia mwisho wa wiki hii  kutoka Sudan baada ya muda wao wa kuishi katika nchi jirani kukamilika.