Libya

Serikali yathibiti tena uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli kutoka kwa waasi

Uwanja wa kimataifa wa ndege wa Tripoli
Uwanja wa kimataifa wa ndege wa Tripoli

Maafisa wa usalama nchini Libya wamefaulu kuchua tena uthibiti wa uwanja wa kimataifa wa ndege jijini Tripoli kutoka kwa waasi waliokuwa wamesabisha kukwama kwa usafiri katika uwanja huo hapo jana.

Matangazo ya kibiashara

Majeshi ya serikali yalijaribu kufanya mazungumzo na waasi kuondoka katika uwanja huo bila mafanikio kabla ya kuamua kutumia nguvu na kuchukua uthibiti wa uwanja huo.

Hata hivyo shughuli za usafari bado hazijarejelewa rasmi tena katika uwanja huo kutokana na barabaraza za uwanja huo kuharibiwa na magari ya waasi hao,na sasa maafisa wa uwanja huo wanasema shughuli zitarejea tena kwa muda wa saa 24 zijazo.

Kundi hilo la waasi lilivamia uwanja huo na kuuzingira kwa madaia kuwa
wanataka kuachiliwa huru kwa kiongozi wao Abu Ajila al-Habshi aliyekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa usalama wa serikali ya mpito.

Uongozi wa serikali ya mpito unaendelea kukabiliwa na changamoto za kuwaunganisha tena wananchi wa Libya baada ya kuangusha utawala wa kiongozi wa zamani wa taifa hilo Muamar Kadhafi aliyeuawa mwaka uliopita.

Wito umekuwa ukitolewa kwa viongozi wa serikali ya mpito kuweka chini silaha  na kudumisha amani baada ya mapinduzi dhidi ya uongozi uliopita.

Baadhi ya waliokuwa wapiganaji  waliofanikisha kuangusha utawala wa Kadhafi wanahisi wametengwa baada ya uongozi mpya kuchua uongozi wa taifa hilo.

Uvamizi huu umetokea wakati Libya ikijiandaa  kuandaa uchaguzi wa wabunge 200 tarehe 19 mwezi huu.