HAGUE

Ocampo asema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limkamate rais wa Sudan Omar Al Bashir

Kiongozi wa mashtaka katika Mahakama ya kimataifa ya ICC Louis Moreno Ocampo anataka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kumwekea masharti magumu rais wa Sudan Omar Al Bashir anayetafutwa na Mahakama hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Sudan katika baraza hilo la Umoja wa Mataifa Daff-Alla Elhag Ali Osman hata hivyo ameshtumu Ocampo kwa kutumia taarifa zisizo sahihi kumshtaki rais Bashir kwa tuhma kuwa alichochea mauji ya maelfu ya watu katika jimbo la Darfur mauji yaliyokamilika mwaka 2005 .

Khartoum aidha inadai kuwa kesi dhidi ya rais wake imechochewa kisiasa suala ambalo Ocampo amesema kuwa ofisi yake itachunguza matamshi hayo ya balozi huyo  wa Sudan.

Ocampo ambaye anastafuu kama kiongozi wa Mashataka katika Mahakama hiyo baadaye mwezi huu, anasema changamoto ya kumkamata rais Bashir iko mikokoni mwa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kulingana sheria ya Rome inayounda Mahakama hiyo, mataifa ya Umoja wa Mataifa ambayo ni wanachama wa Mahakama hiyo wana jukumu la kuhakikisha kuwa wanamkamata mshukiwa yeyote anayetafutwa na Mahakama hiy ,kwa sabbau ICC haina polisi wake.

Hata hivyo Umoja wa Afrika umesema hautamkamata rais Bashir pamoja na waziri wake wa Ulinzi Abdelrahim Mohammed Hussein,  waziri wa zamani wa mambo ya ndani  Ahmed Harun na kiongozi wa kundi la waasi la Janjaweed Ali Kushayb kwa madai kuwa Mahakakama hiyo inawalenga mno viongozi wa bara la Afrika.