NAIROBI

Uwanja wa ndege wa Jomokenyatta jijini Nairobi nchini Kenya wafungwa

Safari za ndege katika uwanja mkubwa wa ndege Afrika Mashariki na Kati wa Jomo Kenyatta jiji Nairobi nchini Kenya zimetatizwa baada ya ndege ya abiria kutoka Misri iliyokuwa inatua kukosa mwelekeo,Jumatano asubuhi katika uwanja huo.

Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo namba 849 ilikuwa na abiria 123 ilikuwa inatua baada ya kuwasili Nairobi kutoka jijini Cairo,baada ya kushindwa kufuata  barabara ya ndege na kukwama lakini hakuna abiria yeyote aliyejeruhiwa katika mkasa huo.

Afisa wa Mawasiliano katika uwanja huo Dominic Ngigi amethibitisha kutokea kwa mkasa huo na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ndege hiyo kushindwa kutua.

Ngingi ameongeza kuwa barabara za uwanja huo zimefungwa kwa sababu za kisualama ,kabla ya shughuli katika uwanja huo kurejelewa tena.

Ndege zote zilizostahili kutua jijini Nairobi sasa zitatua mjini Mombasa ,Entebbe nchini  Uganda na Dar es salaam Tanzania hadi pale hali itakaporejea kawaida.