NIGERIA

Wanamgambo 16 wa Boko Haram wauliwa na majeshi ya Nigeria

Combattants du Mend
Combattants du Mend

Jeshi nchini Nigeria linasema limewaua wanagambo 16 wa Boko Haram Kaskazini mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mauji ya wanamgambo hao yamethibitishwa na Kanali Victor Ebhaleme ambaye anasema wamepambana na magaidi hao katika mji wa Maiduguri Kaskazini mwa taifa hilo.

Makabiliano makali yalizuka kati ya wanajeshi na wanamgambo hao jana Jumanne baada ya wanajeshi kuvamia moja ya kambi ya kundi hilo inayoaminiwa kuwa walikuwa wamejificha.

Mji wa Maiduguri unaelezwa kuwa makao makuu ya Boko Haram ambao wametekeleza mauji ya zaidi ya watu elfu 1 katika mji huo  tangu mwaka 2009 hasa wakilenga Makanisa.

Mbali na hayo mashirika ya kutetea haki za bindamu nchini Nigeria yametuhumu wanajeshi kwa ukiukwaji wa haki za binadamu katika mji huo ikiwa ni pamoja na kuchoma makaazi ya raia na kuwaua raia wasiokuwa na hatia.

Boko Haram ambao wanasema wanapigania ukombozi wa taifa lao dhidi ya elimu ya Magharibi, pia wamekuwa wakisababisha mauji mjini Kano.

Kundi hilo pia limetishia usalama katika majengo ya serikali katika jiji kuu la Abuja pamoja na ofisi za mataifa ya kigeni hasa Marekani.

Serikali ya Nigeria inakabiliwa na hali ngumu ya kulimaliza kundi hilo ambalo makao yake ni Kaskazini mwa nchi hiyo.