SUDAN-SUDAN KUSINI

Sudan na Sudan Kusini wakosa kuafikiana mjini Addis Ababa

Mazungumzo ya amani kati ya Sudan na Sudan Kusini yamemalizika bila ya maafikiano yeyote mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Matangazo ya kibiashara

Mapema juma hili mawaziri wa ulinzi kutoka Sudan na Sudan Kusini walikutana kuzungumzia usalama katika mipaka ya mataifa hayo mawili, pamoja na kuunda eneo la kuyaweka majeshi kutoka pande zote mbili kulinda amani.

Mkutano huo wa siku 10 umemalizika bila ya wajumbe kufahamu ni wapi eneo hilo litabuniwa kama Abyei ,huku Khartoum ikisema Juba inapendekeza eneo ambalo halinashuhudia machafuko zaidi kila mara.

Miongoni mwa maswala mengine nyeti ambayo hayajapatiwa ufumbuzi kati ya mataifa hayo mawili ni kuhusu uraia kwa wananchi wa Sudan Kusini wanaoishi Sudan, ugawanaji wa mapato ya mafuta kabla ya Juba kujitenga mwaka uliopita na mmiliki wa eneo la Abyei lenye utajiri wa mafuta.

Mazungumzo haya yanamazilika miezi miwli baada ya mazungumzo mengine kama haya kutibuka mwezi Aprili,baada ya wajumbe kutoka Khartoum kujiondoa katika mazungumzo hayo.

Umoja wa Afrika chini ya rais wa zamani wa Afrika Kusini Thambo Mbeki, anaongoza mazugumzo hayo.