Waasi wa jimbo la Blue Nile wakabiliana na wanajeshi wa Sudan
Imechapishwa:
Waasi wa Sudan SPLM-N katika jimbo la Blue Nile wamekabiliana na jeshi la serikali, makabiliano ambayo waasi hao wamejigamba kuwaua wanajeshi wa serikali.
Arnu Ngutulu Lodi, msemaji wa waasi hao amesema kuwa wanajeshi wa serikali ya Khartoum walivamia jana Jumapili katika ngome yao na kusisitiza kuwa bado wanaakabiliana nao, maadai amabalo yamekanushwa na msemaji wa jeshi la Sudan Sawarmi Khaled Saad.
SPLM-N ni kundi ambalo bado linapambana na serikali ya Khartoum, ambayo imekuwa ikiilamu Sudan Kusini kwa kutumia waaai hao kusababisha ukosefu wa usalama katika nchi yao.
Maelfu ya watu katika jimbo la Blue Nile wamehama makwao kwa hofu ya kuuawa.