Libya-Mapambano

watu 20 wauawa katika mapigano nchini Libya

Wapiganaji wa NTC nchini Libya
Wapiganaji wa NTC nchini Libya

Watu zaidi ya 20 wameauwa nchini Libya kutokana na makabiliano kati ya kabila la Toubou na majeshi ya serikali mwishoni mwa juma lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa waliopoteza maisha  katika makabiliano hayo ni watoto na wanawake katika eneo la Kufra na kusababisha kujeruhiwa kwa zaidi ya watu wengine 50.

Viongozi wa Jamii ya Toubou wanadai kuwa serikali ya mpito nchini humo inawabagua na eneo lao liko nyuma kimaendeleo, na sasa linatoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuingilia katia na kusaidia jamii hiyo.

Libya imekuwa ikikumbwa na ukosefu wa usalama tangu kuuawa kwa kiongozi wa taifa hilo Muamar Gaddafi mwaka uliopita.

Waasi wenye silaha waliuvamia uwanaja wa ndege mwanzoni mwa juma lililopita na kusabaisha sighuliz ausafiri wa ndege kuparaganyika.