Rwanda-DRCongo

Serikali ya Rwanda yakanusha kuhusika kwake katika mgogoro wa Kivu Kaskazini

Mwanajeshi wa DRCongo
Mwanajeshi wa DRCongo RFI

Serikali ya Rwanda imetupilia mbali tuhuma kuhusu kuhusika kwake katika vurugu zinazoendelea mashariki mwa jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kubaini maskitiko yako kuhusu tuhuma hizo. Hayo yanatokea baada ya serikali ya jamuhuri ya kidemokrais ya congo kuituhumu Rwanda kwa mara ya kwanza katika kuwafadhili waasi wa kundi la M23.

Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa juma lililopita serikali ya Congo ilitowa msimamo wake rasmi kuhusu tuhuma zilizotolewa na Umoja wa Mataifa nchini congo na baadae na shirika la kimataifa linalo tetea haki za binadamu la Human Right Watch kuhusu serikali ya Rwanda kuwafadhili waasi wa kundi la M23 linalo pambana na wanajeshi wa serikali ya Congo.

Msemaji wa serikali Congo Lambert Mende alisema kwamba miongoni mwa waasi 200 na 300 waliotoroka kundi hilo, waliajiriwa kutoka Rwanda na mtandao unajulikana nchini humo. Jambo ambalo linatupiliwa mbali na serikali ya Rwanda ambayo inasema serikali ya Congo Kinshasa inaitumia Rwanda katika kugeuza mtazamamo wa watu kuhusu mzozo wake wa ndani.

Rwanda imekanusha mara kadhaa kuhusika katika harakati za kuwafadhili waasi wa kundi la M23 linaloendesha vurugu katika mkoa wa Kivu kaskazini.

Rwanda ilihusishwa kwa mara ya kwanza katika vurugu hizo, baada ya wapiganaji 11 kutoka kundi la M23 kudai kwamba waliajiriwa kutoka nchini Rwanda. Tume ya mseto iliundwa ili kuwahoji waasi hao, lakini katika ripoti yake ya mwisho ambayo haikuwekwa bayana ambayo iliifikia RFI, nchi hizi mbili hazikuafikiana kuhusu ushuhuda uliotolewa na waasi hao.

Upande wa Rwanda unasema waasi hao hawakutaja uwepo wa wanajeshi wa Rwanda katika kundi hilo aidha gari za jeshi la Rwanda, lakini wamesema waliajiriwa na watu ambao ni raia wa kawaida. Rwanda inasema, kama waliajiriwa katika ardhi yake, ni hatuwa ambayo ilichukuliwa na watu binafsi, haihusishi viongozi. Hata hivyo serikali ya Rwanda imesema kwamba huwezi kuthibitisha kuwa waasi hao 11 ni raia wa Rwanda waliokuwa wakieshi nchini Rwanda