Sudan

Wapinzani waachwa huru nchini Sudani

Kiongozi wa upinzani nchini Sudani Hassan Al Tourab
Kiongozi wa upinzani nchini Sudani Hassan Al Tourab

Viongozi wa upinzani nchini Sudan Ibrahim al-Sonosi na Hassan al-Turabi, hatimaye wameachiliwa huru baada ya kuwekwa kizuizini kwa kipindi cha miezi sita kwa makosa ya kuendelea kuikosoa serikali ya rais Omar Hassan Al-Bashir.

Matangazo ya kibiashara

Sonosi mwenye umri wa miaka 70 pamoja na mwanasiasa mwingine wa upinzani Ali Shamar walizuiliwa katika uwanja wa ndege wa Khartoum mwishoni mwa mwaka uliopita baada ya kutua kutokea nchini Kenya na kukamatwa bila ya kuaabiwa lolote.

Viongozi hao wa upinzani pia walishtumiwa kuwa na uhusiano wa kundi la waasi la Justice and Equality Movement katika jimbo la Darfur, suala ambalo wamekiri na kusema kuwa lengo lao ni kutaka waasi hao kuungana na serikali.

Aidha wapinzani hao wameshtumiwa pia kuwa katika mawasiliano ya karibu na maafisa wa serikali wa Sudan Kusini.