Misri

Mahakama ya kikatiba nchini Misri yampasisha mgombea Ahmed Chafik wakati huo huo yafuta bunge

Wanaharakati wakiandamana nchini Misri
Wanaharakati wakiandamana nchini Misri REUTERS/Suhaib Salem

Mahakama nchini Misri imeamuwa kutomfuta Ahmed Chafik mgombea kiti cha urais anaepingwa na wananchi kwakuwa aliwahi kuhudumu katika serikali ya rais alieondolewa madarakani Hosni Mubarak kama waziri mkuu, siku mbili tu kabla ya kuitishwa kwa duru ya pili ya uchaguzi mkuu wa rais. Mahakama hiyo imefuta pia bunge la nchi hiyo, hali ambayo inachochea moto zaidi kwa wananchi wanaendelea kuandamana.

Matangazo ya kibiashara

Umuzi huo wa mahakama ya kikatiba nchini Misri umetolewa jana wa kumruhusu Ahmed Chafik kuendelea katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa rais unaotarajiwa kufanyika Jumamosi na Jumapili hii.

Sheria iliotolewa na bunge nchini humo mwezi April iliopita, ilikataa washirika wa rais wa zamani Hosni mubaraka kuwania cheo chochoye nchini Misri katika kipindi cha miaka 10, na baade kuamuwa kupelekwa mahakamani sheria hiyo. Hatimae mahakama hiyo imepinga sheria hiyo na kumruhusu Ahmed Chafik kuendelea katika kinyang'anyiro hicho.

Ahmed Chafik ambae aliwaahidi wananchi kwamba utawala wa zamani ni wa zamani, hivyo atawajibika zaidi, atapambana na Mohamed Morsi wa chama cha Muslim Brodherhoods. Iwapo Ahmed Chafik angeliondolewa kwenye duru hiyo ya pili ya uchaguzi, basi uchaguzi ungelifutwa, wakati ambapo chama cha muslim Bradherhoods kilikuwa kimeongoza katika duru ya kwanza.

Uongozi wa chama cha kisiasa nchini Misri Muslim Brothderhood wanaonya kuwa hali ya kidemokrasia nchini humo,inaelekea pabaya baada ya Mahakama ya rufaa nchini humo kutangaza kutupilia bali uchaguzi wa wabunge uliofanyika mwaka uliopita.

Mahakama ya ki katiba nchini Misri imesema ilitoa uamuzi huo baada ya kubaini kuwa sheria ya uchaguzi wa wabunge hao kuvunjwa ambapo wabunge wengi wa Muslim Brotherhood walichaguliwa katika nafasi za wagombea binafsi.