TANZANIA

Mahama kuu nchini Tanzania yaamuru kusitishwa kwa mgomo wa madakatari.

Mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari Tanzania dokta Ulimboka Steven.
Mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari Tanzania dokta Ulimboka Steven. magangaone.blogspot.com

Mahakama kuu kitengo cha kazi nchini Tanzania imeamuru kusitishwa kwa mgomo wa madaktari uliopangwa kuanza leo kutokana na madhara makubwa yatakayotokana na mgomo huo.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama imetoa amri hiyo kufuatia madakatari kujiapiza kuanza mgomo usio na kikomo hii leo kufuatia kushindwa kufikia muafaka na serikali katika kuboresha maslahi yao.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa mgomo huo umesitishwa mpaka hapo madai ya serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya mwaka 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) na kutaja sababu za msingi za kusitisha mgomo huo kuwa ni pamoja na madhara yasiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha .