ADDIS-ABABA-ETHIOPIA

Mahakama ya Ethiopia yawakuta na hatia za ugaidi watu 24

Reuters

Mahakama kuu nchini Ethiopia imewakuta na hatia ya makosa ya ugaidi watu ishirini na nne akiwemo kiongozi wa juu wa upinzani na mwandishi wa habari wa siku nyingi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Akisoma uamuzi wa mahakama hiyo jaji Endeshaw Adane amesema kuwa mahakama imewakuta na hatua mwandishi wa habari Eskinder Nega na kiongozi wa upinzani Andualem Arage pamoja na watu wengine 22 wanaotuhumiwa kushirikiana na kundi moja la Marekani la Ginbot 7.

Kwa mujibu wa sheria ya masuala ya ugaidi nchini humo watu hao wanakabiliwa na adhabu ya kunyongwa ingawa upande wa mashataka umeomba watu haio wahukumiwe kifungo cha maisha.

Wakati huohuo Maharamia wa kisomali waliokuwa wamewateka wanandoa wawili raia wa Afrika kusini wamewaachia huru baada ya kuwa inawashikilia kwa zaidi ya miezi 20.

Debbie Calitz na Bruno Pelizzari walitekwa mwaka jana mwezi wa kumi na maharamia hao wakati wakisafiri kutumia bahari ya hindi na kudai kuwa walinyanyaswa kibinaadamu na maharamia hao.

Polisi nchini Somalia wamethibitisha kuachiwa kwa wanadoa hao na kusema kuwa waliachiwa baada ya kufanyika operesheni maalumu kati ya vikosi vya serikali na vile vya Umoja wa Afrika AMISOM.