MALI-SENEGAL

UNESCO yaonya kutoweka kwa Mji wa Timbuktu, Wananchi Senegal kuchagua wabunge

RFI

Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulika na masuala ya utamaduni, sayansi na elimu, UNESCO limeonya kuhusu kutoweka na kuharibika kwa mji wa Timbuktu ambao upo kwenye orodha ya urithi wa dunia.

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo limesema kuwa kuutaja mji wa timbuktu na maeneo mengine ya kumbukumbu kwenye mji huo kuwa kwenye hatari inalenga kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanalindwa kutokana na uharibufu unaoendelea kujitokeza wakati huu ambapo kuna mapigano.

Profesa Baba Akib Haidar ni mtaalamu wa makumbusho ya tumbukut ambaye anakubaliana na tanagazo la UNESCO na kusema hali ya usalama angalau imeanza kurejea kwenye eno hilo.

Katika hatua nyingine wananchi wa Senegal Jumapili ya wiki hii watashiriki zoezi la upigaji kura za wabunge kwenye uchaguzi wa kwanza ambao utashuhudia wanawake wengi zaidi wakiwania nafasi za uwakilishi ndani ya bunge la nchi hiyo.

Uchaguzi hui unakuja baada ya kupita miezi mitatu toka nchi hiyo ifanye uchaguzi wa rais na kumteua Macky Sall aliyemaliza utawala wa miaka 12 ya rais Andoulaye Wade ambapo sasa rais Sall aliahidi kutekeleza katiba ya nchi hoyo kwa kutoa nafasi nyingi kwa wanawake.

Zaidi ya wagombea elfu saba watashiriki ichaguzi huo ambapo vyama vya muungano vimetoa majina zaidi ya 24 ya wanawake watakaowania nafasi hizo siku ya jumapili.

Katiba ya Senegal inataka usawa wa kijinsia ndani ya bunge la nchi hiyo.