RWANDA-DRCONGO

Rwanda yaridhika na mkutano wa ICGLR

Serikali ya Rwanda imekiri mkutano wa nchi Wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR uliomalizika mwishoni mwa juma lililopita nchini Uganda umekuwa na mafanikio kitu ambacho kitasaidia kupatikana kwa amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amesema mkutano huo umelata matumaini mapya lakini akatumia fursa hiyo kupuuza madai ya Kinshasa kutokana na nchi hiyo kuondoa wanajeshi wake.

Louise Mushikiwabo

 

 

 

 

 

 

Madai ambayo yametolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda yanapuuzwa na serikali ya Kinshasa kupitia Msemaji wake Lambert Mende Omalanga.

Lambert Mende
Lambert Mende

 

 

 

 

 

Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC zimeendelea kutofautiana kimsimamo tangu Kinshasa kuituhumu Kigali kufadhili Waasi wa M23.