NIGERIA

Wananchi Nigeria wawalalamikia wanajeshi kwa kufyatua risasi

Reuters/Eduardo Munoz

Wakazi wa Mji unaokumbwa na Machafuko ulioko Kaskazini mwa Nigeria, Maiduguri, wamewashutumu Wanajeshi kwa kitendo cha kufyatua risasi na kuua watu kadhaa hapo jana baada ya gari lililokuwa likitumika kufanyia doria kulipuliwa kwa Bomu.

Matangazo ya kibiashara

Vikosi vilielekea katika eneo la tukio lilipolipuliwa gari hilo, mlipuko ambao pia ulisababisha takriban wanajeshi wawili kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa Mashuhuda watukio hilo, wanajeshi walitumia fimbo zao na vitako vya bunduki kupiga Raia, hali iliyosababisha hamaki na vurumai kupamba moto ambapo nyumba na Maduka vilichomwa moto.

Makundi yanayotetea haki za binaadam vimeshutumu jeshi kwa kutumia mabavu katika kutekeleza wajibu wao hasa wanapokuwa wameshambuliwa
Mji wa Maiduguri, unaelezwa kuwa ngome ya kundi la Kiislamu la Boko Haram, wanaoshutumiwa kuua watu zaidi ya 1400 katika eneo la kaskazini na Katikati ya Nigeria, tangu mwaka 2010.

Hayo yanatokea wakati Serikali ikitafuta mbinu za kukabiliana na matukio ya kigaidi yanayotekelezwa na kundi la Boko Haram katika maeneo mbalimbali nchini humo.