SUDAN

Mashirika ya misaada yasimamisha misaada nchini Sudan kwa kuhofia usalama

Reuters

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotoa msaada kwenye jimbo la Kordofan na Darfur nchini Sudan yameeleza kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo. 

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya mashirika hayo yanakuja kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara ambayo yemekuwa yakiwalenga wafanyakazi wake na wanajeshi wanaolinda amani nchini humo.

Juma hili kumeripotiwa kuwa serikali ya Sudan imefanikiwa kuwakamata watu kadhaa kuhusiana na tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa wanajeshi wanne wa Nigeria.

Wanajeshi hao walikuwa wakilinda amani na kushambuliwa tukio ambalo sasa limezusha hofu zaidi ya kiusalama kwenye miji hiyo.

Hata hivyo majeshi ya UNAMID hayakuweza kuthibitisha taarifa hizo iwapo ni kweli watu hao wamekamatwa.

Ali al Zatari ni mwakilishi mkaazi wa Umoja wa Mataifa mjini Kordofan na ameeleza wasiwasi wao kuhusu usalama wa wafanyakazi wake wanaotoa misaada kwenye jimbo hilo na kwamba wamelazimika kusimamisha huduma zao kwa muda.