Habari RFI-Ki

Usalama mipakani mwa nchi za Afrka Mashariki na Kati si salama

Sauti 09:24
RFI

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limefanikiwa kuwakamata raia ishirini wa Ethiopia ambao wanatajwa kuingia nchini kwa njia haramu baada ya kufanyika msako katika eneo la Pwani ya Bahari ya Bagamoyo.Raia hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisio na sasa wanatarajiwa kupandishwa kizimbani hii leo kutokana na kosa la kuingia nchini kwa njia zisizo halali ambapo wenyewe wamekiri kufanya hivyo mbele ya Idara ya Uhamiaji. Kutokana na hali hiyo makala ya Habari Rafiki hii leo inajikita katika kuangalia usalama katika mipaka kwenye nchi za Afrika Mashariki.