ETHIOPIA

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam afanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri

REUTERS/Tiksa Negeri

Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ametangaza kufanya mabadiliko kwa mara ya kwanza kwenye baraza lake la mawaziri ambalo limedumu kwa muda mrefu toka utawala wa marehemu Meles Zenawi aliyeaga dunia mwezi Augosti mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumzia mabadiliko hayo waziri mkuu Desalegn amesema kuwa yanalenga kutengeneza viongozi vizazi vijavyo ambao ni wachapa kazi na wataleta mabadiliko nchini humo, hatua ambayo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa anataka kujumuisha vijana kwenye serikali yake.

Miongoni mwa mabadiliko ambayo ameyafanya ni pamoja na kumteua waziri mpya wa mambo ya nje, Biashara na manaibu mawaziri wakuu wawili, ambapo waziri wa afya aliyehudumu kwa muda mrefu kwenye serikali ya nchi hiyo ndio anapewa jukumu la kuongoza wizara ya mambo ya kigeni ya Ethiopia.

Wakati huohuo kiongozi wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria amepongeza umoja uliopo kati ya makundi ya Jihadi yanayopigana na serikali mbalimbali duniani kwa lengo la kuutetea Uislamu.

Kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia, kundi hilo limetoa mkanda wa viedo ukimuonesha kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau akizungumza kwa lugha ya kiarabu huku akipongeza umoja ambao umeoneshwa na makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali duniani.

Kiongozi huyo ameyaonya mataifa ya Marekani, Uingereza na Israel kwa kuendelea kukashifu Uislamu na kuapa kundi lake kuendelea na mashambulizi zaidi nchini Nigeria.